Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, makala iliyoandikwa na Dkt. Nadia Hassan wa Chuo Kikuu cha York imeeleza kwamba; maadui wa Uislamu wanatumia fursa ya chuki dhidi ya Uislamu kwa manufaa yao, na wanaikandamiza kwa mfumo maalumu kila aina ya shughuli zinazounga mkono Palestina.
Dkt. Hassan, akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Ottawa, alisema: “Baada ya mwaka 2023, ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu nchini Kanada vimeongezeka kwa kiwango kikubwa mno.” Kulingana na Taasisi ya Strategic Dialogue, kufikia Oktoba 29 mwaka huu, idadi ya machapisho na hotuba zinazobeba ujumbe wa chuki imeongezeka kwa asilimia 422%.
Kesi nyingi za malalamiko zimepokelewa kote Kanada, mfano mmoja ni tukio la mwanamke Mwislamu wa Ottawa aliyeshambuliwa na mtu mmoja wakati akihudhuria maandamano ya kuiunga mkono Palestina; mshambuliaji huyo alimvua kwa nguvu hijabu yake.
Chuo Kikuu cha York kimezitaka taasisi zote za elimu ya juu kuunda mazingira huru kwa wanafunzi na kutozuia sauti zao, inatarajiwa vyuo vikuu viwe mahali salama ambapo wanafunzi wanaweza kueleza mitazamo yao kuhusu masuala ya Palestina bila woga.
Chanzo: 5 Pillars
Maoni yako